"Nimeamini kikulacho ki nguoni mwako, nitagombea nafasi hii, wajumbe kama mnataka kunitoa mnitoe kwa heshima, niitwe Baba wa Taifa wa TLP, nikifa wanachama mnizike vizuri, lakini sitaachia nafasi hii hawa, nitakula nao sahani ama zao, ama zangu" Augustine Mrema.
"Alichokifanya Mrema leo ni kutuchafua ili wanachama watuone hatufai, lakini wajumbe wanaona hilo, kama nimeandikiwa kupata uenyekiti nitaupata tu, lakini asihusishe kupanda kwangu daladala, hayo ni maisha yangu binafsi, bora yangu ninayepanda daladala kuliko yeye anayekaa kwenye nyumba ya TLP na kutegemea ruzuku za chama ili aishi" Benedict Mutungirehi.
Mrema anaishi Sinza, Dar es Salaam, anatembelea gari aina ya Toyota Landcruiser
Mutungirehi ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Kyerwa mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment