Wednesday, April 22, 2009

Dk Slaa Vs Waziri Ghasia

"Tunawajua wabunge wezi wa nyaraka,na wamo humu humu ndani, na hata ninavyoongea wananisikia, waache. wapo wanaotumia nyaraka za wizi kwa lengo la kutaka kujijengea umaarufu wa kisiasa" Waziri Hawa Ghasia jana bungeni mjini Dodoma.
"Kama ni kutishwa nilishatishwa mpaka na Rais Kikwete, na kuna watu walikuwa wakinitishia hata kifo lakini siyumbishwi katika kulitetea taifa langu. Nasisitiza, raia wema wachukue hizo nyaraka kwenye makabati ya Serikali waniletee"Dk Wilbroad Slaa, jana nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
"Mbunge kuiba nyaraka za Serikali ni wizi na halina uhusiano na kinga yake bungeni, Mbunge yeyote akikutwa na nyaraka za Serikali atakuwa ametenda kosa la wizi" Waziri Ghasia jana bugeni Mjini Dodoma.
"Ghasia hajui anazungumza nini, lakini mimi ninawaomba Watanzania wenye dhamira ya dhati na nchi yao waendelee kuniletea nyaraka hizo na mimi nitazitumia bungeni kwa sababu hakuna sheria inayomkataza Mbunge kusema ukweli kwa maslahi ya nchi yake" Dk Slaa nje ya ukumbi wa Bunge mjini Doidoma , Jana.

No comments:

Post a Comment