Friday, February 6, 2009

Watafiti hawa waje bongo

Katika kila wafanyakazi watatu mfanyakazi mmoja anatumia kompyuta za ofisini uangalia video za ngono katika muda wao wa kazi kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa wafanyakazi wa maofisini nchini Uingereza.

Theluthi ya wafanyakazi wa maofisini chini Uingereza wanaangalia video za ngono kwa kutumia kompyuta za ofisini katika muda wao wa kazi.

Katika asilimia hiyo 33 ya waliokiri kuangalia video hizo zisizofaa katika muda wao wa kazi, ni asilimia 7 tu kati yao walikiri kufumaniwa wakati wakiangalia video hizo za ngono.

Utafiti huo pia ulibainisha kuwa zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa maofisini nchini Uingereza walirudi maofisini wakiwa wamelewa baada ya kwenda mapumziko ya chakula cha mchana.

Utafiti huo ulizidi kubainisha kuwa wafanyakazi wengine walikuwa wakinywa pombe kabla ya kuingia kazini huku asilimia 31 wakishindwa kuhudhuria vikao vya kikazi kwakuwa walikuwa wakiendelea na ulabu katika vilabu vya pombe.

Asilimia 62 ya wafanyakazi wa maofisini walithibitisha kutongozana na wafanyakazi wenzao wakati wa kazi.

Asilimia 28 ya wafanyakazi ambao hawakuwa wapenzi wa pombe au video za ngono walikiri kupitiwa na usingizi kwenye meza zao wakati wa kazi.

Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya ulinzi wa Email ya Proofpoint ulibainisha pia kuwa robo ya wafanyakazi walikosea na kuwatumia wafanyakazi wenzao meseji za kimapenzi walizolenga kuwatumia wapenzi wao.

Utafiti huo ulifanywa kwa wafanyakazi zaidi ya 400 katika maofisi mbali mbali nchini
Uingereza.

No comments:

Post a Comment