Monday, February 9, 2009




Picha ya juu ni kifaa kilichokutwa chumbani kwa Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa(Chadema) katika hoteli iitwayo Fifty Six mjini Dodoma
Picha ya Chini ni Ofisa wa Polisi akikagua kifaa hicho, EDIC- Mini Tiny. Kwa mujibu wa polisi imethibitika kuwa ni cha kurekodia sauti na hakina uwezo wa kupiga picha.
Kwa mujibu wa polisi, kifaa kama hicho kilikutwa pia katika chumba cha Mbunge wa Konde, Dk Ali Taarab Ali(CUF), uchunguzi zaidi unaendelea.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Omary Mganga, amesema Polisi pia wamepeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali mvinyo uitwao Altar Wine aliopelekewa Dk Slaa kama zawadi.
Sakata hilo limekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali na linapewa nafasi kubwa kwenye vyombo kadhaa vya habari nchini

No comments:

Post a Comment