Friday, February 6, 2009

Mwisho wa darasa, maisha yanaendelea


LEO ni siku ya mwisho ya mafunzo kuhusu uandishi wa habari wa kisasa (Modern Journalism) yaliyoanza Jumatatu wiki hii.

Tangu Jumatatu mimi na wenzangu kutoka vyombo mbalimbali vya habari tulikuwa tukipata ‘darasa’ kuhusu mambo mbalimbali tuliyokuwa tukiyafahamu kidogo au ambayo hatukuyafahamu kabisa yanayohusiana na modern Journalism hasa Online Journalism.

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuhudhuria mafunzo haya hapa TGDLC, kwenye majengo ya chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam.

Nimejifunza mambo mengi ninayoyahitaji kwenye utekelezaji wa majukumu yangu katika taaluma hii, na kwa ujumla yamekuwa na manufaa makubwa kwangu.

Kwa mfano, nilikuwa nafahamu namna ya kutumia mtandao wa internet lakini sasa upeo wangu umepanuka, nafahamu mambo mengine kuliko nilivyokuwa nafahamu awali, na nimeongezewa nyenzo nyingine ya kuwa karibu na jamii.

Katika maisha yangu sikutarajia kama kuna siku nitakuwa na BLOG, nilikuwa napata taarifa nyingi kwenye blogs ‘magazeti tando’ ya watu mbalimbali, na sikuamini kama na mimi ningeweza kufanya kama wao, kweli hakuna kisichowezekana.

Mafunzo yameniwezesha kuwa miongoni mwa bloggers Tanzania, kupitia anuani simulizi.blospot.com nawashururu wote walionipa moyo, nitajitahidi kuwa karibu nao kadiri nitakavyoweza, tuombeane heri.

Mkufunzi, Peik Johansson kutoka Kampuni ya Utangazaji ya Finland ametuekeleza mambo mengi, na nimefurahi zaidi kwa kuwa yamekuwa ni shirikishi, anasema jambo, unafanya papo hapo.

Mwandishi wa habari mwandamizi, Maggid Mjengwa naye katuekeleza mengi kuhusu blogs, tumefahamu tunapaswa kufanya nini, kwa vipi, na tumeelezwa pia changamoto mbalimbali tutakazokabiliana nazo wakati tukiwasiliana kwa njia hiyo.

Mmoja wa wadau wa mafunzo haya, Rose Haji ametueleza kuwa, kundi letu ni la kwanza mwaka huu, ni la tatu tangu yalipoanza, yalianza mwaka jana, yataisha mwakani.
Ni mafunzo yanayotolewa kupitia programu ya miaka mitatu, kutakuwa na kundi lingine mwaka huu kutoka vyombo vingine vya habari

No comments:

Post a Comment