SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani alighafilika aliposema kuwa Bunge linaingilia Mahakama.
Spika Sitta amesema leo bungeni mjini Dodoma kuwa, alichokisema Jaji Mkuu sivyo, na kwamba, Bunge lina mamlaka ya kuingilia shauri lolote linalomhusu Mbunge na mtu mwingine.
Kwa mujibu wa Spika Sitta, Ibara ya 100, ibara ndogo ya kwanza ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa madaraka hayo kwa Bunge na hakuna mtu au chombo chochote chenye uwezo wa kuhoji kauli ya Mbunge anayoitoa bungeni.
No comments:
Post a Comment