BUNGE leo litatoa msimamo kujibu kauli ya Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani kwamba chombo hicho cha kutunga sheria kinaingilia majukumu ya mahakama.
Spika wa Bunge, Samuel Sitta jana alitoa mwelekeo wa msimamo wa Bunge kwa kusema kuwa Mahakama imekuwa ikitoa uamuzi usiozingatia maslahi ya umma.
“Hapa watasema pia naingilia mahakama….potelea mbali” alisema spika Sitta bungeni.
Watanzania wanasubiri msimamo huo wa Bunge na kwa ujumla hatma ya mitazamo tofauti ya mihimili hiyo miwili ya dola ili wafahamu tunakwenda wapi.
No comments:
Post a Comment