Watuhumiwa wawili wanaodaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 221 leo wamefikishwa Mahakama Kuu Tanzania jijini Dar es Salaam kusilikiza jibu la ombi lao la kupunguziwa masharti ya dhamana.
Watumishi hao wa zamani wa Benki Kuu Tanzania Amitus Liumba na Deogratius Kweka wameiomba mahakama hiyo iwapungizie masharti ya dhamana ili waweze kudhaminiwa.
Jaji wa Mahakama kuu, Protas Rugazia ameahirisha kesi hiyo hadi Ijumaa, wamerudishwa rumande.
No comments:
Post a Comment