Thursday, February 12, 2009

Ni kweli Mwana FA kaacha kazi?




HABARI ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinjuma maarufu kwa jina la Mwana FA ameacha kazi katika Benki ya NBC.
Mwana FA alikuwa akifanya katika kitengo cha bima makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, alianza kazi hapo baada ya kumaliza masomo katika Chuo Cha Usimamizi wa Fedha(IFM) kilichopo jijini humo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mzee wa Bado Nipo nipo Sana anajindaa kwenda kusoma nje ya nchi hivyo huenda atasitisha shughuli za muziki hadi atakapomaliza masomo.
Hadi mwanzoni wa wiki hii, msanii huyo na rafiki yake wa karibu, Ambwene Yesayah maarufu kwa jina la AY walikuwa Uingereza kwa shughuli za muziki.

No comments:

Post a Comment