Thursday, February 12, 2009

Shahada zinauzwa dola 2,000

WAHADHIRI wanane waandamizi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wana Shahada za Udaktari ambazo ni bandia au walizipata katika taasisi zisizotambulika kimataifa.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Mayunga Nkunya amesema, hivi karibuni mamlaka hiyo ilibaini kuwa baadhi wadhahiri katika chuo hicho walikuwa na Shahada zinazotiliwa mashaka.

Kwa mujibu wa Profesa Nkunya, ulifanywa uchunguzi kuthibitisha mashaka hayo na kwamba, TCU imewasilisha serikalini matokeo ya uchunguzi huo.

Amesema, anafahamu kuwa baadhi ya taasisi za nje zinauza shahada kwa dola 2,000 au zaidi ambazo ni sawa na takribani sh milioni 2.7 za Tanzania.

No comments:

Post a Comment