Friday, February 6, 2009

Malezi White House



MKE wa Rais wa Marekani, Michelle Obama amewakataza watoto wake, Malia na Sasha wasichanganye na 'masupastaa' wa Marekani katika njia mojawapo ya kuwafanya watoto wake waishi maisha ya kawaida.

Mara ya mwisho watoto hao kujichanganya na masupastaa wa Marekani ilikuwa Januari 20 mwaka huu wakati wa sherehe za kuapishwa kwa baba yao kuwa Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika.

Malia mwenye umri wa miaka 10 na Sasha mwenye umri wa miaka 7 walijivinjari na nyota kadhaa wa muziki na sinema wakati wa sherehe hizo.

Kwa kuzingatia kauli ya Michelle,wanawe hawatakutana na "A-list" wa Marekani akiwamo Beyonce ambaye walitumia muda mwingi naye wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita wa Marekani.

Watu wa karibu wa familia hiyo walilieza gazeti la Us Weekly kwamba mke wa Obama ameamua wanawe waishi maisha ya kawaida hapo White House jijini Washington.

Kabla ya kuhamia hapo, Obama na familia yake walikuwa wakiishi Chicago,kuna taarifa
kwamba,Malia na Sasha wamehamishwa shule.

"Michelle anatumia muda mwingi kuzungumza na binti zake kuhusiana na shule yao mpya na
marafiki zao wapya katika shule hiyo" alisema rafiki mwingine wa familia ya Obama.

Us Weekly lilisema kuwa Michelle hana mpango wa kukodisha mtu wa kuwaangalia binti zake kwa kuwa bibi yao Marian Robinson, 71, ameishahamia ikulu kusaidia kuwaangalia wajukuu zake.
--------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment