Tuesday, February 10, 2009

Msajili wa vyama vya siasa upo?




Kuna mdau katuma ujumbe huu anaomba msaada wako,anasema

Nimekuwa nikitatizwa sana haswa ninapoona huu utitiri wa matawi ya vyama vya Siasa haswa vya Tanzania kufungua matawi nje ya nchi na haswa nchi za magharibi na India.

Sijawahi kusiki chama cha Labour, Republicans wala Democrats wamefungua tawi Tanzania au maeneo mengine nje ya nchi zao.

Hivi ni sifa zipi mtu anapaswa kuwa nazo ili akubaliwe kuwa mwanachama huko ughaibuni? Je ni kwa mtu aliye mtanzania tu au hata aliyeukana uraia wake anaruhusiwa?

Kama mtu ameukana uraia wa TZ na kujibandika wa USA au UK nadhani si mtanzania tena huyo na hivyo moja kwa moja anapoteza stahili yake.

Hofu yangu ni kuwa na wanachama wa vya vyama vyetu vya siasa ambao si wa-Tanzania na hivyo kupoteza ile maana halisi ya vyama vyetu kwa kuwa vyama vinavyofungua matawi huko vimesajiliwa Tanzania.

Hivyo ni kusema kwamba yeyote yule pasipo kujali uraia wake anaweza kujiunga na chama chetu au kuanzisha tawi popote pale duniani apendapo. Kitu hiki hakiniingii akilini kabisa.

No comments:

Post a Comment