LEO ni siku mbaya kwa wapenzi wa muziki wa dansi Tanzania kwa kuwa wamepata taarifa zizonasikitisha na kuwaumiza.
Sikuwahi kutarajia kwamba, ipo siku umma wa Watanzania utatangaziwa kuwa moja ya bendi kongwe zaidi za muziki huo nchini, DDC Mlimani Park Orchestra imevunjwa!
Naamini taarifa hizi zimewaumiza wengi kwa kuwa huwezi kusimulia historia ya muziki wa dansi nchini bila kuitaja DDC Mlimani Park wana Sikinde Ngoma ya ukae waliokuwa wakiporomosha burudani kwenye uwanja uwanja wao wa nyumbani,DDC Kariakoo a.k.a Old Trafford.
Waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1978, Shirika la Uchumi la Jiji la Dar es Salaam(DDC) wametangaza kuufunga mradi huo hivyo sikinde hawapo tena.
Uongozi wa DDC umesema, wafanyakazi wote wa DDC Mlimani Park wamepunguzwa kazi kuanzia Februari 6 mwaka huu, na kwamba ajira zao zitakoma Machi Mosi mwaka huu.
Baadhi ya wanamuziki nyota waliokuwa katika bendi hiyo ni Shaaban Dede, Hassan Rehani Bitchuka, Karama Regesu, John Ngosha, Eddo Sanga, Hassan Kunyata na Abdallah Hemba.

No comments:
Post a Comment