Wednesday, February 4, 2009







Mke wa Obama Kiboko!

MKE wa Rais wa Marekani, Michelle Obama(45) amevunja ukimya kwa kusema ya moyoni mwake
kuhusu yeye 'kumpiga tafu' mumewe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na
hatimaye sasa wanaishi White House.
Kwa mara ya kwanza,Jumanne wiki hii Michelle alihutubia akiwa mke wa Rais wa Marekani
akasema kipaumbele chake cha kwanza kilikuwa 'Mom-chief' wa Marekani.
Michelle na familia yake walihamia White House Januari 20 mwaka huu,amesema ingawa wanaishi
huko hatakuwa akikaa nyumbani tu.
Obama na Michelle wana watoto wawili wa kike, Malia(10) na Sasha(7), Rais aliyemtangulia,
George W. Bush naye alikuwa na watoto wawili wa kike,Jenna na Barbara.Rais aliyewatangulia,
Bill Clinton alikuwa na mtoto mmoja wa kike, Chelsea.
Usikose kusoma historia ya maisha ya Michelle Jumamosi wiki hii ili ufahamu pia namna
alivyokutana na kuanza uhusiano wa kimapenzi na Barack Obama.
-------------------------------------------

No comments:

Post a Comment