PUA ya mfalme wa miondoko ya POP, Michael Jackson(50) ipo hatarini kudondoka na akabiliwa na matatizo mengine ya kiafya yanayohatarisha maisha yake.
Mtaalamu wa tatizo la kiafya linalofahamika kama MSRA, Mark Enright amesema,Jackson anahitaji tiba haraka kwa kuwa tatizo hilo haliwezi kutibiwa na antibiotics.
Hivi karibuni hospitali ya Beverly Hills ilisema kuwa, mwanamuziki huyo pia anasumbuliwa na tatizo la ngozi.
Taarifa kuhusu kuzorota kwa afya ya gwiji hilo pop zimekuwa zikiongezeka, mwishoni mwa mwaka jana mmoja wa watu wake wa karibu walisema anasumbuliwa na ugonjwa wa kijenetiki uitwao A1AD uliosababisha jicho lake la kushoto lipoteze nguvu ya kuona kwa asilimia 95.
Mwandishi wa taarifa za maisha ya Jackson, Ian Halperin amesema, mwanamuziki huyo alikuwa akizungumza kwa taabu na kwamba, pia alikuwa akisumbuliwa na tatizo sugu la kuvuja damu ndani ya mwili liitwalo kitalaamu, Gastrointestinal ambalo lingeweza kumuua.
Kwa mujibu wa Halperin, Jackson anakabiliwa na upungufu wa protein uliosababisha mapafu yaharibike, hivyo anahitaji kubadilishiwa mapafu.

No comments:
Post a Comment