MAHAKAMA Kuu Tanzania imekataa ombi la waliokuwa watumishi wa Benki Kuu Tanzania (BOT) la kupunguziwa masharti ya dhamana yanayowataka wajidhamini kwa Sh bilioni 55 kila mmoja au kuweka dhamana ya mali isiyohamishika/zisizohamishika zenye thamani hiyo.
Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Projestus Rugazia leo amewaeleza washitikakiwa hao, Amatus Liyumba na Deogratius Kweka kuwa uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ulikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai
Liyumba na Kweka wanatuhumiwa kuidanganya Bodi ya BOT hivyo kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 221. Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.
No comments:
Post a Comment