Friday, February 6, 2009

Wanaume wale nini?

KUNA mdau anauliza ni vyakula gani zinazofaa kuliwa na wanaume ili wawe na nguvu na stamina wakati wa kufanya tendo la kujamiiana.

Kwa mtazamo wake,ni muhimu jamii ikajadili suala hilo kwa madai kuwa takwimu zinaonyesha kwamba ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wanawake wanakosa huduma ya tendo la ndoa kwa ufasaha kiasi cha kutotosheka!!

Anasema, anafahamu baadhi ya mambo kama vile ukosefu wa mazoezi ya kutosha, ulevi, na mafuta mengi mwilini pia vinachangia wanaume kutotimiza haja za wake zao

Anahitaji kuelimishwa ni vyakula gani iwe vya kupikwa au vyakula asilia vinavyoweza kumsaidia mwanaume 'kutimiza wajibu wake?'vya muda mrefu (sex boosters) na vya muda mfupi kabla ya kufanya tendo (stimulators)?

Wakati anasubiri jibu la maswali hayo naomba pia kujibiwa kama mwanamke naye hahitaji kula vyakula fulani ili kumuwezesha kuridhika sana au kuridhika haraka wakati wa kujamiiana.

Pia si vibaya nikiuliza, jambo la msingi ili mwanamke aridhike ni kiasi cha muda anaotumia kufanya tendo hilo au namna yeye na patner wake wanavyofanya? jibu kwa bmsongo@hotmail.com
Majibu yako yatachapishwa kwenye blog hii.

2 comments:

  1. Swali hilo waulize mafataki maana ndio wenye kukimbizana na vimwana kil wakati ila maswali mazuri maana hiyo hoja ni issue muhimu

    ReplyDelete
  2. wale mfugo kwa wingi kaka mambo yatakuwa safiiiiiii

    ReplyDelete