WATU sita wakiwamo wanafunzi wawili wa shule mbili za sekondari mkoani Tanga wamekufa papo hapo baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiiria aina ya Toyota Hiece kugongana uso kwa uso la lori lililokuwa limebeba saruji.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Muheza Mkanyageni mkoani humo, watu 11 wamejeruhiwa, wane hali zao ni mbaya.
Taarifa kutoka Tanga zimeeleza kuwa maiti wote wametambuliwa.
No comments:
Post a Comment