Wednesday, April 13, 2016

Askofu Mathias Isuja afariki dunia


Askofu Mstaafu wa jimbo Katoliki Dodoma, Mathias Isuja amefariki dunia jana usiku, Itigi mkoani Singida.

Taarifa za uhakika ni kwamba, Askofu Isuja amefariki dunia katika hospitali ya misheni Itigi.
 
Kiongozi huyo kanisa aliyepata daraja la upadre Desemba 24, 1960 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Askofu Isuja alizaliwa Agosti 14, 1929 katika kijiji cha Haubi wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma. 

Isuja alipewa daraja la upadre Dodoma akiwa na umri wa miaka 31.

Aliteuliwa kuwa askofu Juni 26, 1972 akiwa na umri wa miaka 42 na kusimikwa Septemba 17, 1972, Dodoma. 

Askofu alistaafu Januari 15, 2005 akiwa na umri wa miaka 75.

No comments:

Post a Comment