Friday, May 1, 2015

JK- Ningekuwa msanii wa Bongo flava

Dakika chache zilizopita, Rais Jakaya Kikwete amewaeleza wananchi kuwa, kama asingekuwa Rais, angekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la Bongo flava.

Rais ameyasema hayo katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani, Mei Mosi.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, Rais Kikwete ameimba wimbo wa Mimi msafiri bado nipo njiani, sijui lini nitafika, naulizia watu kule ninapokwenda, naambiwa bado ni mbali.

No comments:

Post a Comment