Friday, May 1, 2015

Diamond- Nilianza kumtongoza Zari kwenye ndege


zarMsanii wa muziki wa kizazi kipya anayedaiwa kuwa na mafanikio zaidi kibiashara hivi sasa, Nassib Abdul a.k.a Diamond, na mpenzi wake, Zarina Hassan a.k.a Zari the Boss leo wametoa ya moyoni kwa kueleza namna wanavyopendana na walivyokutana.

Diamond amesema, alikutana na Zari kwenye ndege wakati wanatoka Afrika Kusini, akarusha ndoano na hadi sasa ni wapenzi.

Kwa mujibu wa Zari, ilichukua muda kukubali kuwa mpenzi wa msanii huyo, lakini hatimaye akasema YES.

Zari ni mjamzito na ana watoto watatu wenye umri wa miaka 11, 10 na minane.

Mfanyabiashara huyo amesema, wanawe wanaishi Afrika Kusini na wanafahamu kuwa yupo na Diamond.

Diamond anasema, Zari kuwa na watoto watatu si tatizo kwake.

No comments:

Post a Comment