Friday, October 17, 2014

TSN Supermarket kufungua tawi lingine Dar

 

Kampuni inayomiliki maduka ya TSN maarufu kwa jina la TSN Supermarket kesho Jumamosi (Oktoba 18) inatarajiwa kufungua tawi lingine jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mikakati yake kusogeza huduma kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Koiya Kibanga, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa tawi la Kijitonyama.

Kwa mujibu wa Kibanga, katika uzinduzi huo kutakuwa na burudani ikiwemo ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava), Hamisi Mwinjuma a.k.a Mwana FA.

Kwa habari zaidi tembelea www.tsngrouptz.com
Displaying TSN Supermarket Opening Soon Final Final.jpg 



No comments:

Post a Comment