Wednesday, October 15, 2014

Kikwete- Sijui ningesema nini

“Napenda niweke wazi, naipongeza Katiba hii kwa kumuenzi Mwalimu Nyerere, sijui ningesema nini leo (maadhimisho ya kifo cha Nyerere), kama Katiba hii ingependekeza Katiba ya mfumo wa Serikali tatu,” 

 “Kwa kweli hii ni Katiba bora, ni zaidi ya Katiba nzuri, ni bora kuliko Katiba tuliyo nayo, hii ya sasa imeboreshwa sana, inatambua na kuimarisha tunu za taifa letu.” 

“Nawaambia hii ndio Katiba hasa ya wananchi, ombi langu kwenu jiandaeni vyema na kujitokeza kupiga kura ya maoni ili tuweze kupata Katiba hii bora, naombeni pia muwe na subira kwa kuwa wakati wowote mtapewa utaratibu kuhusu upigaji wa kura hiyo ya maoni,”

Rais Jakaya Kikwete

No comments:

Post a Comment