Monday, September 8, 2014

Mbunge- Niliuza karanga sasa nataka urais

 “Siyo lazima uwe mtoto wa tajiri ndiyo uoneshe kipaji chako. Hili peke yake linanipa sababu ya ziada ya kwa nini nitamani kuota kuwa Rais – nataka niwe mfano hai wa mafanikio ya Ndoto ya waasisi wa Taifa letu, kuwa sote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuna haki na fursa sawa bila kujali nani anatokea familia ipi.”

 “Ndiyo maana, natangaza rasmi sasa kuwa ninatia nia ya kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2015,” alisema na kuamsha hoihoi, nderemo na vifijo kutoka kwa wafuasi wake.

“Mimi ninaamini kwamba, kama hata mimi nimefika hapa kutokana na kuishi maisha ya kimasikini, ya kuuza karanga na samaki mitaani, ya kwenda shule pekupeku, basi kila mtanzania anaweza, na ana haki ya kufika hapa na kwenda mbele zaidi yangu. Mafanikio siyo haki ya wachache, ni tunu ya Mwenyezi Mungu kwa kila mtu. Ninaamini ni haki ya kila mtanzania kuota ndoto yake, kuifanyia kazi na kuifikia,” 

Dk Hamisi Kigwangalla

No comments:

Post a Comment