Monday, August 11, 2014

Shibuda afunguka

"Uongozi ni kutanguliza hekima na busara katika kufikia
uamuzi, uongozi si Magereza na hata Magereza wafungwa wana haki zao, Tundu Lissu amekuwa nani katika nchi hii… 

anaongea kama kasuku
hafanyi utafiti anakurupuka na kuongea na kutoa matamko?  Mie nitamtaka athibitishe tuhuma hizo anazozitoa dhidi yangu. Nasema Chadema si baba wala mama yangu,"


"Muislamu hawezi kutetea Uislamu kama hajui nguzo saba za Uislamu na pia huwezi kuwa Shekhe bila kupitia Madrasa na hata katika Ukristo,

huwezi kuutetea Ukristo kama hujui Biblia na hukusoma mafundisho… na mie siwezi kuwa Ukawa wakati sijaelimishwa kuhusu kundi hilo,” 

"Mie niliingia Chadema kwa hiari yangu baada ya kuona dhuluma zilizokuwa ndani ya CCM, chama kilichonilea kisiasa, nikaona heri niende Chadema ambako nilidhani kuna demokrasia na ukombozi wa kweli, lakini nilichokikuta humo ni tofauti kwani kila siku wazee wangu mnasikia napata misukosuko isiyo na maana,"

 "Pamoja na shutuma zote zinazotolewa juu yangu na kupachikwa majina mbalimbali kuwa mie ni ‘Msaliti’ mara ni ‘Pandikizi la CCM’, lakini hata siku moja sijawahi kuitwa katika Kamati Kuu ya Chadema na kuhojiwa. 

“Nimekuwa nikitukanwa hadharani na vijana wa Chadema mbele ya viongozi wa juu wa chama, hawachukui hatua… mie mtu mzima hapo natafsiri kuwa wametumwa na viongozi hao ili kunifanyia fitna hizo,"

Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda

No comments:

Post a Comment