Friday, June 6, 2014

Mpoki- Siongei na waandishi hadi nife

 
Kuna taarifa zinazodai kuwa mchekeshaji aliyepata umaarufu kupitia kipindi cha televisheni  cha Ze Comedy, Mujuni Sylvester 'Mpoki' ametangaza kwamba, hataongea na waandishi wa habari kwa kuwa HAWANA AKILI.

Inadaiwa kuwa, Mpoki AMEAPA kuwa, hatazungumza na waandishi wa habari na anaamini atabaki na msimamo huo kwa MAISHA YAKE YOTE.

Inadaiwa kuwa Mpoki ameamua hivyo baada ya vyombo vya habari kumkosoa baada ya msanii huyo kuwatukana wasanii na waalikwa wakati akiwa mshehereshaji 'MC' kwenye hafla ya utoaji Tuzo  za Muziki  za Kilimanjaro kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Tanzania Daima, Juni 06, 2014

No comments:

Post a Comment