Saturday, June 7, 2014

Mbunge Nassari kuoa leo


MBUNGE wa Arumeru Mashariki , Joshua Nassari leo anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nnko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo sherehe ya harusi itafanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
 
 Nassari amealika watu wote wakiwemo wananchi katika jimbo la Arumeru Mashariki na hawatatakiwa kuwa na kadi.


Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru
 
"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!" alisema Nassari.


 Chanzo: mwanahabarihuru

No comments:

Post a Comment