Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimpongeza Samuel Sitta baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba
“Jamani kunichagua mimi ni kama kumrejesha chura
kwenye dimbwi la maji alilolizoea. Msiwe na wasiwasi ataogelea tu na
ninawaahidi kuwa ikiwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu, mtanichagua
nitawatumikia kwa uaminifu, sitakubali upendeleo wa aina yoyote,
nitasimamia kanuni tulizozipitisha hapa,”
“Nitawaongoza kwa utumishi
uliotukuka na uadilifu ili tupate Katiba bora, yenye viwango na kwa
wakati. Nina hulka ya kuwapenda wale ninaowaongoza, kwa hiyo nitakuwa
mtetezi wa shughuli mbalimbali…Ninawaahidi Watanzania kutenda haki na
kuwapatia Katiba yenye viwango na kwa wakati.
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta
No comments:
Post a Comment