Tuesday, August 27, 2013

Dada wa Mbowe- Sikuwa Chadema kifamilia

DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, wakati anajiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitoka Chadema. Baada ya kukabidhi kadi ya Chadema katika ofisi za CCM Wilaya ya Hai Grace alisema.
 
“Nimeamua kwa hiyari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.
Picture: Grace Mbowe, Hassan Mtenga
 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga akimkabidhi , Grace Mbowe, kadi ya CCM.
 
“Kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
 

No comments:

Post a Comment