Sunday, May 19, 2013

Mwanzilishi JamiiForums mahututi

maxence-melo-ajali
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali
Wanaodaiwa kuwa ni wanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali

 
Kuna taarifa zinazodai kuwa, mmoja wa wanaodaiwa kuwa ni waanzilishi na wamiliki wa Jamii Forums, Maxence Melo, amepata ajali ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza; kilometa chache kutoka Nzega mjini.
Mwanzilishi mwenzie na anayetajwa kuwa ni Msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema Maxence na ndugu yake ambaye naye alikuwepo kwenye ajali hiyo, walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu na uchunguzi zaidi. 

  Mushi amesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana. 
 
Haijaelezwa Bw. Maxence melo ameumia kiasi gani, ila taarifa zinasema kuwa ndugu yake amejeruhiwa vibaya .
Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokuwa wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.
 
Blog ya Lukaza

2 comments:

  1. zamakia@gmail.comMay 20, 2013 at 3:54 PM

    nawatakia afya njema.mungu awape nafuu ya haraka waweze kupona.

    ReplyDelete
  2. zamakia36@gmail.coMay 20, 2013 at 4:56 PM

    mungu awape nafuu ya haraka.wapate nguvu.wakalitumikie taifa

    ReplyDelete