Sunday, May 19, 2013

Mfanyabiashara Arusha auawa kwa risasi ClubMFANYABIASHARA wa Arusha, Ayoub Mlay, ameuawa kwa kupigwa risasi katika club ya usiku iitwayo, Ambrosia iliyopo Mbezi, Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amesema, mfanyabiashara huyo alipigwa risani saa 10 alfajiri leo katika mazingira ya ulevi.

Kwa mujibu wa RPC Kenyela, kijana ambaye ni Mhasibu, Conrad Leo, anadaiwa kumpiga risasi Mlay baada ya kutokea ubishani kati yao. 

Bado haijafahamika ni kwa nini Conrad alikwenda Club na bastola, na haijathibitishwa pia endapo anaimiliki kihalali.

Mwili wa marehemu Mlay ulipelekwa katika hospitali ya Mwananyamala.

No comments:

Post a Comment