Sunday, April 28, 2013

Kijana anajisi kuku jike

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma
Mwanaume aitwaye Yusuph Bakari (28) mkazi wa kata ya Kigera Manispaa ya Musoma amenajisi kuku jike na kumsababishia 'maumivu makali'

Akizungumzia tukio hilo, Mamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Absalom Mwakyoma amewaambia waandishi wa habari kuwa Aprili 24 saa tatu asubuhi Bakari 'alifanya mapenzi' na kuku jike na kuumuumiza.
 
Kuku huyo ni mali ya bibi Nyamera Kitambara (76).

Mwakyoma amesema, bibi huyo kushuhudia kuku wake akinajisiwa, kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kumkamata kijana huyo, alipiga kelele, wananchi wakaenda na kumkamata Bakari na kumfikisha katika kituo kidogo cha polisi Kigera .

No comments:

Post a Comment