Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape 
Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa CCM 
uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza
KATIBU
 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 
amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo lazima kitakufa kwa sababu ya laana ya ubaguzi.
Ameitaka Chadema isitafute mchawi nje ya chama hicho kwa kuwa ubaguzi ulioota mizizi ndiyo unaowamaliza hivyo waandae mazishi kwa kuwa hakuna namna ya kuinusuru Chadema.
Nape aliyasema hayo Januari 20, 2013, jijini Mwanza kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa mpira wa Nyamagana.
"Hamuwezi kuwa na chama ambacho ili kiongozi wake adumu na kuheshimika lazima awe anatoka ukanda fulani au ukoo fulani ndio adumu, vinginevyo anasukiwa mizengwe na mwisho kutimuliwa" alisema Nape na kuongeza "walianza na kina Chacha Wangwe na Watanzania wote wanajua leo kilichompata Chacha Wangwe, sasa wameanza kumwandama Zitto na wanaoitwa vijana wake, na pia nasikia wamejipanga kumfukuza Shibuda wiki ijayo."
"Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alishasema dhambi ya ubaguzi ni kubwa, na ni sawa na kula nyama ya mtu, ambapo mtu akishaila anazoea kiasi kwamba haachi, basi nao Chadema hawana namna ya kuachana na ubaguzi unaoendelea ndani ya chama chao, hivyo watasambaratika kwa laana hiyo ya Mwalimu", alisema Nape.
" Ikiwa wanabaguana ndani ya kichama kidogo kiasi hichi ambacho hakijai hata mkononi, watafanyaje wakipewa dhamana ya kuongoza hata kipande cha nchi yetu?" alihoji.
"Sasa leo nimeamua kuwapa ushauri wa bure kabisa Chadema wasiendelee kutafuta mchawi nje ya chama chao", alisema.
No comments:
Post a Comment