Monday, October 15, 2012

Watu 15 mbaroni mauaji ya RPC Mwanza

Kamanda Liberatus Barlow
Kuna taarifa kwamba, hadi jana jioni watu 15 walikuwa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zilizopatikana jijini Mwanza zinaeleza kwamba, idadi hiyo ya watuhumiwa waliokamatwa huenda ikaongezeka kuanzia leo Jumatatu, baada ya marehemu Barlow kuagwa jijini Mwanza.

 Jeneza lenye mwili wa Kamanda Liberatus Barlow

Mwili wa kiongozi huyo mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pia unatarajiwa kupelekwa nyumbani kwake Dar es Salaam , na baadaye utapelekwa  nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.



Kuna taarifa kwamba, upelelezi wa kina na wa hali ya juu unafanyika kote nchini, ikiwa ni pamoja na maeneo ya mipakani ili kuwanasa watuhumiwa wa mauaji hayo.
Kamanda Barlow aliuawa usiku wa kuamkia Jumamosi kwa kupigwa risasi eneo la Kitangiri jijini Mwanza muda mfupi baada ya kumshusha mwanamke aliyefahamika kuwa ni Mwalimu jijini humo. 

No comments:

Post a Comment