Thursday, October 25, 2012

Viongozi wapya UVCCM

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
Mjumbe wa Kamati Kuu, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akiwa na Mwenyekiti mpya wa UVCCM,  Khamis Sadifa Juma na Makamu Mwenyekiti mpya wa umoja huo, Mboni Mhita.
 Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti UVCCM Beno Malisa akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa.
Kamanda wa Chipukizi Kingunge Ngombale-Mwiru akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama wakati wa kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa UVCCM.
Katibu Mkuu wa UVCCM Martine shigela akimkaribisha meza kuu Khamis Sadifa Juma.
Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, Khamis Sadifa Juma.
Blog za mikoa

No comments:

Post a Comment