Picha ya hapo juu inaonyesha wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), wanaomuunga
mkono Mwenyekiti mpya wa Taifa wa Umoja huo, Khamis Sadifa Juma na
viongozi wenzake, wakimtwanga mmoja wa wanachama waliojitokeza kumpinga
mwenyekiti huyo kwa mabango , wakati alipowasili makao
makuu ya umoja huo Dar es Salaam, akitoka mkoani Dodoma
Shamrashamra za kumpokea Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM) , Khamis Sadifa Juma jijini Dar es Salaam jana
ziligeuka uwanja wa vita baada ya makundi yanayopingana kuchapana
makonde.
Tafrani hiyo ilianza baada ya kundi moja la vijana waliokuwa wanane kutokea likiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kupinga ushindi wa mwenyekiti huyo, wakati utambulisho wa ugeni huo ukiendelea katika ofisi za makao makuu ya UVCCM, zilizopo jijini Dar es Salaam.
Baada ya kundi hilo kujitokeza na mabango yao, ndipo vijana wa upande wa Mwenyekiti (Juma), walipoanza kuwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata

Kukiwa hakuna msaada wa Polisi, vijana hao walilishambulia kundi hilo
kwa muda, huku baadhi yao wakitiwa nguvuni na vijana hao na kuingizwa
katika ofisi ya UVCCM huku waandishi wa habari wakizuiwa kuwahoji
watuhumiwa wala kuingia ndani ya ofisi hiyo.
‘’Hatutaki waandishi humu ndani, tokeni na asiingie mtu, hawa tutashughulika nao wenyewe, wanatusumbua mno hawa kwa siku nyingi,” alisikika mmoja wa vijana hao akiongea kwa sauti ya juu.
‘’Hatutaki waandishi humu ndani, tokeni na asiingie mtu, hawa tutashughulika nao wenyewe, wanatusumbua mno hawa kwa siku nyingi,” alisikika mmoja wa vijana hao akiongea kwa sauti ya juu.
Sherehe hizo hazikuhudhuriwa na kiongozi yeyote wa kitaifa wa CCM
Habari kwa hisani ya Kamanda wa Matukio
No comments:
Post a Comment