Sunday, October 28, 2012

Padre aliyezama baharini kuzikwa Iringa

Mwili wa Mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Consolata, nchini Tanzania, Padre Salutaris Lucas Massawe utazikwa Jumanne ijayo katika Parokia ya Mshindo mkoani Iringa.

Padre Massawe, alikufa kwa kuzama baharini Oktoba 25 katika ufukwe wa Bagamoyo mkoani Pwani.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyKP6r7vn5v3sWFXIYuvne-6umFjboWoGDIvs9bu0NyMt3zJZ53Acn1Jxbqcf34G6d0TNRHy61ROOjRZDE9gODGU8KutVoD-jzgGxNz3BcCMOEyqhbEM8BirQxw-bkJnNONEP7rP-e8RQ/s1600/P.+Lelo.jpg

Kiongozi huyo wa kiroho na wanashirika wenzake walikwenda Bagamoyo kupumzika baada ya mkutano wa wakuu wa Shirika la Waconsolata Barani Afrika, uliokuwa unafanyika Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Oktoba 26 mwaka huu, Padre Leonard Maliva wa Shirika la Consolata Mako makuu Iringa, alisema, Padre Massawe aliishi katika Parokia ya Consolata Mshindo, na atazikwa huko.
Kabla ya kuwa mkuu wa shirika hilo, Padre Massawe pia alifanya kazi za kimissionari nchini Ethiopia, Kenya, na Italia. 

Septemba 7, 2011 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Waconsolata nchini Tanzania hadi alipokufa Oktoba 25, 2012.
 
Marehemu Padre Salutaris Massawe alizaliwa kunako tarehe 8 Julai 1962, Jimbo Katoliki la Moshi. 

Alisoma shule ya Msingi Singachini kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1978 na baadaye akaendelea na masomo yake ya Sekondari Maua Seminari kati ya Mwaka 1980 hadi mwaka 1985. 
 
Aliendelea na masomo ya Falsafa na Taalimungu kwenye Chuo cha Waconsolata kilichoko mjini Nairobi kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1988.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, kunako tarehe 27 Juni 1993 alipewa daraja takatifu la Upadre na Askofu Amedeus Msarikie wa Jimbo la Moshi wakati huo. 

No comments:

Post a Comment