Ujumbe alioacha marehemu Oscar John (24)
Kijana Oscar John (24) mkazi wa mkoa wa Dodoma amejinyonga kwa pazia hadi kufa baada ya kuhisi kuwa amemuua mchumba wake kwa kumkata kata kwa
kisu.
Oscar
alijinyonga chumbani kwa mchumba wake Maria Chilinde (25) ambaye ni
mfanyakazi wa chuo cha VETA mjini Singida.
Kabla ya kukatisha uhai wake, kijana huyo alimkata kata Maria kwa
kutumia kisu.
Kablaya kujiua Oscar aliandika ujumbe ufuatao
‘mimi Oscar John nimekufa pamoja
na Maria,hela elfu tisini pamoja na simu zangu watachukua wazazi
wangu.By by wapendwa wote’.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa chuo cha VETA mjini Singida Afridon Mukhomoi, Oscar huenda aliandika ujumbe huo baada ya kudhani kuwa amemuua
Maria na alipomaliza kuuandika, alijitundika kwenye kenchi kwa kutumia
pazia na kusababisha kifo chake.
Amesema ameelezwa kuwa, baada ya Maria kuzirai na Oscar kuhisi kuwa amekufa , alimfunika msichana huyo kwa shuka na kuandika ujumbe huo.
Inadaiwa kuwa Oscar aliamua kumuua Maria baada ya wazazi wa msichana huyo kudai mahari ya shilingi milioni mbili ili amuoe binti yao, Oscar alishindwa
kumudu kiwango hicho na hivyo kuamua wote wafe.
Blog za mikoa
No comments:
Post a Comment