Saturday, September 1, 2012

Askofu Paschal Kikoti kuzikwa leo


 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda kabla ya kuupokea mwili wa marehemu Askofu Paschal Kikoti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, aliyefariki dunia Jumanne ya Wiki hii kutokana na shinikizo la damu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza
Ndege iliyouleta mwili wa marehemu Paschal Kikoti baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda.
Mapadri wa Kanisa Katoliki wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda Paschal Kikoti mara baada ya kuteremshwa kwenye ndege.
Waumini wa kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda wakiwa wamelazwa kwenye ukumbi wa kanisa  Katoliki Jimbo la mpanda baada ya kupoteza fahamu baada ya mwili wa Askofu wa Jimbo la Mpanda Paschal Kikoti ulipofikishwa kwenye Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo la Mpanda.

No comments:

Post a Comment