Thursday, August 30, 2012

Hawa Ngulume afariki dunia

(Picha na blog ya Daily Mitikasi)
 
Aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali kwa vipindi tofauti, Hawa Ngulume amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa baadaye.

Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani  kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment