Askofu
Paschal William Kikoti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini
Mwanza alikokuwa amelazwa.
Makamu wa Askofu wa Jimbo la Mpanda, Padri Patrick Kasomo
amekaririwa akisema, kifo cha Askofu Kikoti kimetokana na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa Padri Kasomo, mwili
wake utawasili kesho Alhamisi kwa taratibu za mazishi.
Padri
Kasomo amesema, mwili wa Askofu Kikoki unatarajiwa kuzikwa Jumamosi wiki hii kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria mjini
Mpanda.

No comments:
Post a Comment