Thursday, May 31, 2012

Wenje- Mbatia kafungishwa ndoa ya mkeka

Mbunge wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Wenje (CHADEMA) amemshambulia Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akidai amefungishwa ndoa ya mkeka na CCM.

Wenje amwaaeleza wananchi wa Kata ya Majengo mjini Mtwara kuwa, Mbatia ni Mbunge wa Viti maalum kwa kuwa ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete ili kumsaidia kutekekeza ilani isiyotekelezeka.

  Wenje amesema, kitendo cha Mbatia kukubali ubunge wa viti maalumu, kimeonesha udhaifu wake mkubwa.

Amemponda kuwa, mwanasiasa huyo si mpinzani wa kweli wa kupinga ufisadi na ubadhirifu unaofanywa na Serikali ya CCM.

Hatua hiyo ya Wenje kumuita Mbatia Mbunge wa Viti maalumu, iliibua mvutano katika mkutano huo kwa kuwa, watu walitofautiana, wengine wakisema hata CHADEMA kuna wabunge wa viti maalumu.

  Mwisho wa mkutano huo, Wenje alitoa ufafanuzi namna wabunge wa viti maalumu wa chama wanavyopatikana na wabunge wanaoteuliwa na rais kwa mujibu wa mamlaka ya ibara ya 66 (1) (a) ya katiba ya nchi.

“Ndugu zangu hakuna sababu ya kubishana hapa, wapo wabunge wa viti maalumu wa chama husika wanaotokana na idadi ya wabunge halali waliochaguliwa kwa kura za wananchi, na wapo wabunge wa kuteuliwa na rais kwa mujibu wa kifungu hicho, wote ni wabunge, lakini tofauti yao ni huyu ni wa rais na huyu ni wa wananchi"

No comments:

Post a Comment