WATU wanne wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa Singida, baada ya basi la Mohamed Trans, kugongana na basi dogo jana (Jumatano) mjini Singida.
Kamanda
wa Polisi mkoa Singida, Celina Kaluba, amesema chanzo cha ajali ni
uzembe wa dereva basi la Mohamed Trans, aliyetaka kuingia katika
barabara kuu ya Mwanza- Dodoma, bila kuchukua tahadhari yoyote.
Waliojeruhiwa ni dereva wa basi dogo na abiria wake, dereva wa basi la Mohamed Trans lenye namba za usajili, T 848 BEQ alitoroka.
Majeruhi
waliolazwa ni Yesaya Samson (dereva wa basi dogo) aliyevunjika miguu
yote, Paulo Rajabu, Parick Stephano na William Richard, waliopata
majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.
Abiria
zaidi ya 50 waliokuwa kwenye basi la Mohamed Trans hawakupata madhara.
Basi la Mohamed Trans lilikuwa likitoka Morogoro kwenda Mwanza, basi dogo lenye namba za usajili T 499 BRS
Dyana, lilikuwa likitoka Singida mjini kwenda kijiji cha Iglansoni, Singida
vijijini.
No comments:
Post a Comment