Thursday, May 17, 2012

Mchezaji Simba apata ajali, aaga dunia

MCHEZAJI mahiri wa Simba, Patrick Mutesa mafisango amekufa alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam.

Mchezaji huyo 'kiraka', ameaga dunia muda mfupi baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Tazara.

Mafisango alikuwa na uwezo wa kucheza namba 6, 8, 10 na hata 11.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, Mafisango alipata ajali hiyo wakati akiendesha gari, na kwamba, alikuwa anamkwepa mwendesha pikipiki.

Rage amesema, wakati anamkweka mwendesha pikipiki, gari hilo liliingia mtaroni, mchezaji huyo raia wa Rwanda akaumia sana, na aliaga dunia muda mfupi baadaye.

Amesema, Mafisango alikuwa na rafiki yake, na mtu mwingine, na kwamba, wameumia.

Mafisango ameaga dunia siku chache baada ya kocha wa timu ta taifa ya Rwanda kumuita katika timu ya taifa ya nchi hiyo.


No comments:

Post a Comment