Wednesday, May 30, 2012

Rais Kikwete na mgeni wake, Rais wa Ivory Coast



Rais Jakaya Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo Mei 30, 2012.
 
Rais huyo wa Ivory Coast amekuja kuhudhuria mkutano wa afDB utakaofunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC, Arusha. 
 
Rais Jakaya Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast wakiwa katika picha ya pamoja katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo. 
 
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment