Sunday, May 27, 2012

Chadema yafunika Dar es Salaam

Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana vilifurika umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Umati huo ulianza kuingia uwanjani hapo asubuhi huku kukiwa na vibanda 16 vilivyokuwa vikisimamiwa na vijana kutoka vyuo vikuu ambao ni wanachama wa CHADEMA kwa ajili ya watu kujiunga na chama hicho na wengine kurudisha kadi za vyama vingine.

012

Mewnyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA , Freeman Mbowe, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho leo katika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya VUA GAMBA VAA GWANDA
ambayo itazunguka mikoa yote ya Tanzania
.
 
Dr Wlbroad Slaa nae akitoa msisitizo juu ya kampeni hiyo ya VUA GAMBA VAA GWANDA.
Mbunge wa Ubungo John Mnyika akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoa msisitizo kuhusu kampeni ya Vua Gamba Vaa Gwanda.
Wafuasi wa CHADEMA wakiwa wamefurika katika viwanja vya Jangwani
jijini Dar es Salaam



Picha zote kwa hisani ya blog ya Full Shangwe

  Watu 3,124 walijiunga na CHADEMA jana katika viwanja hivyo akiwemo aliyekuwa kada maarufu wa CCM, mzee Raphael Koimere.
 
Mkutano ulifunguliwa kwa dua kutoka kwa viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo na kisha baadhi ya viongozi wakaanza kuzungmza huku viongozi watatu wakiwa ndiyo wasemaji wakuu katika mkutano huo, ambao ni Freeman Mbowe, Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaonya watu aliowaita wasaliti ndani ya chama hicho, kwa kuwataka wajirudi mara moja, vinginevyo watashughulikiwa  kwa  mujibu wa taratibu.

 Hivi karibuni Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda amekuwa akizozana na viongozi wa chama hicho tangu pale alipotangaza nia yake ya kuwania urais huku akimtaja Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwa atakuwa meneja wake wa kampeni.  
Bila kumtaja jina, Mbowe alianza kwa kutoa kauli zilionekana moja kwa moja kumjibu Shibuda, akisema wapo watu wanaodai kuwa Chadema ni chama cha udini na ukabila na kusisitiza kuwa huo ni uzushi.

Wakati akiendelea kusema hayo, umati uliokuwepo uwanjani hapo ulipokea kauli hiyo kwa kupaza sauti kwamba  “Shibuda ang’olewe …Shibuda ang’olewe… Shibuda aondoke!’ hoja iliyojibiwa na Mbowe papo kwa hapo  kwamba  mkutano huo haukuwa na lengo la kumng’oa mtu.

“Sikuja hapa kumng’oa mtu…Tumng’oe?” Alihoji Mbowe  na kuongeza: “Ngoja nitoe kauli ya chama. 
Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee.”  
Alisisitiza kuwa chama hicho kimejengwa kwa zaidi ya miaka 20 na  kimeweza kujenga ngome katika mikoa ya Mwanza Lindi na Mtwara.   
Huku akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyoitoia miaka ya 1960, Mbowe alilitaka Jeshi la Polisi kutowatisha wanachama wa Chadema na kuonya kuwa wakifanya hivyo, wananchi nao watajibu mapigo.   
“Chadema kitakuwa chama cha mwisho kuvuruga amani nchini. Nawaonya kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na kama Mwenyekiti wa Chadema na kama Mbunge. Nawaomba polisi, waache kuwasumbua wana Chadema,” alionya  Mbowe.   
Licha ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani, watu walianza kufurika katika Viwanja vya Jangwani kuanzia saa 8:00 mchana.  
Kampeni ya Movement for Change(M4C)  Akizungumzia mkakati huo, aliwataka wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla kujitolea kukichangia fedha ili kufanikisha kampeni hiyo kwani alisema kukiondoa CCM madarakani si kazi rahisi, inahitaji  gharama kubwa.

 “Kila mwananchi anawajibu wa kubadilisha maisha yake. Kila mtu anapaswa kuwa wakala wa mabadiliko. Kuiondoa CCM kuna gharama kubwa, kule Arumeru watu walichanga kile walichokuwa nacho  kuanzia Sh. 50 na kuendelea na tulishinda, au siyo? Tusije tukapata viongozi kwa fedha chafu,” alisema.  
Mbowe pia alisisitiza kuwa watakuwa makini na wanachama wa CCM wanaohamia Chadema akisema kuwa watatakaswa kwanza kabla ya kupewa uanachama. 


1 comment:

  1. safiiiiiiiiiiiiiiiii sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete