Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo imemtangaza John Mnyika kuwa ni Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo.
Hukumu hiyo imetolewa muda mfupi uliopita, na hali ni shwari katika eneo la Mahakama, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema, Mahakama imetenda haki, na watafanya mkutano mkubwa wa hadhara Jumapili jijini Dar es Salaam.
Kesi hiyo namba 107 ya mwaka juzi ilifunguliwa na
aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng’humbi
akipinga matokeo yaliyompa ushindi Mnyika katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kwa
madai taratibu na sheria ya uchaguzi zilikiukwa.
Katika
kesi hiyo, Ng’humbi ana hoja tano za msingi ambazo ni kuwepo kwa tuhuma za
kashfa kuwa aliuza jengo la Umoja wa Wanawake, kubadilishwa kimakosa kwa kura katika
fomu za matokeo ya ubunge, kuwepo kwa watu kimakosa katika chumba cha
majumuisho ya kura .
Hoja
nyingine ni matumizi ya kompyuta za Mnyika wakati wa majumuisho ya kura na
ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika uchaguzi huo ambao ulisababisha kuwepo
kwa kura hewa 14,854 .
Kwa
mujibu wa ushahidi uliotolewa na upande wa mdai, katika fomu ya matokeo jumla
ya kura halisi zilizoandikwa ni 119,823 lakini ukijumlisha kura za wagombea
wote unapata kura 132,493 na ukitoa kura halisi na jumla ya kura za wagombea
zinabaki kura 14,854.
Wakili
wa Ng’humbi Issa Maige alidai kuwa licha ya upande wa wadaiwa kukiri kuwepo kwa
kura hewa zaidi ya 14,000 ulishindwa kutoa maelezo ya kina na ufafanuzi kuhusu
hizo kura zilitoka wapi na kuiomba Mahakama kubatilisha matokeo hayo.
No comments:
Post a Comment