Monday, April 2, 2012

Kijana aliyeiba kuku achagua kula kinyesi kuepuka kifo

Mkazi wa Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Musa Mwambapa (25), amelazimishwa kula kinyesi cha binadamu baada ya kukamatwa ameiba kuku katika Kijiji cha Sisitila, Mkoani humo.


Inadaiwa kuwa, tukio hilo lilitokea Machi 30 mwaka huu, nne asubuhi katika kijiji hicho wakati mtuhumiwa alipoiba kuku mali ya Vedastus Jerome (45).


Baada ya mtuhumiwa kukamatwa wananchi wenye hasira walimtaka achague adhabu moja kati ya mbili, ambazo ni kumwagiwa mafuta ya petroli kisha kuchomwa moto au kula kinyesi cha binadamu.


Kijana huyo alichagua kula kinyesi cha binadamu, akala kisha akaachiwa.


Chanzo: Blog ya Chimbuko letu

No comments:

Post a Comment