Monday, April 2, 2012

Chadema yashinda Arumeru

Mshindi wa ubunge katika uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akizungumza leo asubuhi baada ya kutangazwa mshindi.


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Arumeru Mashariki.


Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru, Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA , Joshua Nassari kuwa mshindi baada ya kupata kura 32,672, mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw Sioi Sumari amepata kura 26,757.


Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo, DP kura 77, NRA kura 35, AFP kura 139, UPDP kura 18, TLP kura 18 na SAU kura 22.


Kwa mujibu wa Kagenzi , zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha, waliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696, kura halali zilikuwa 60,038, na zilizoharibika ni kura 661.

No comments:

Post a Comment