Mwili wa kijana gwiji wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba unazikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Muda mfupi uliopita mwili wa marehemu Kanumba umetolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, unapelekwa katika viwanja vya Leaders, Kinondoni kwa ajili ya ibada na baadaye wananchi watatoa heshima za mwisho.
Hadi hivi sasa, viwanja vya Leaders vimejaa, na inatarajiwa kwamba, eneo hilo litafurika mamia ya watu wanaokwenda kuuaga mwili wa Kanumba.
Msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ (18) bado yupo Polisi na anatarajiwa kushitakiwa upelelezi utakapokamilika kuhusu chanzo cha kifo cha Kanumba.
Lulu anahusishwa na kifo cha Kanumba kilichotokea saa sita usiku wa kuamkia Jumamosi nyumbani kwake (kwa Kanumba) Sinza, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amesema Polisi wanaendelea kuchunguza kubaini chanzo cha kifo cha k
Kanumba.
“Inaonesha chanzo cha ugomvi wao ni wivu hasa kutokana na Lulu kutoka nje kwenda kuzungumza na simu, hivyo tunafanya uchunguzi wa mawasiliano ya simu na uchunguzi wa kisayansi kwa vielelezo vingine tulivyokuta eneo la tukio kama vile, mvinyo, soda na panga kama vilitumika.
No comments:
Post a Comment